TAARIFA KWA AJILI YA MKUTANO WA KUITAMBULISHA “LAKE VICTORIA BASIN TOURISM EXPO 2019” KWA VYOMBO VYA HABARI UTAKAOFANYIKA KWENYE UFUKWE WA KABUHARA, KATA YA KANYANGEREKO, BUKOBA VIJIJINI, SIKU YA JUMATATU TAREHE 18 NOVEMBA, 2019

  • Home
  • /
  • TAARIFA KWA AJILI YA MKUTANO WA KUITAMBULISHA “LAKE VICTORIA BASIN TOURISM EXPO 2019” KWA VYOMBO VYA HABARI UTAKAOFANYIKA KWENYE UFUKWE WA KABUHARA, KATA YA KANYANGEREKO, BUKOBA VIJIJINI, SIKU YA JUMATATU TAREHE 18 NOVEMBA, 2019
on 26 Nov 2019 8:29 PM

Waheshimiwa Madiwani wa Kata za Maruku na Kanyangereko,
Viongozi wa Dini mlioko hapa,
Washirika wetu: Kabuhara Beach; Clouds Media Group; Tanzania Airports Authority (TAA); CRDB Bank na TANAPA
Mzee Pius Ngeze; Mzee wetu Mashuhuri wa Mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla;
Ndugu Ally Nchahaga – Mkurugenzi wa Vision Investments ambao ndio Event Managers wetu,
Ndugu Wanahabari,
Mabibi na Mabwana,
Habari za asubuhi!
Awali ya yote ninapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu aliye mwingi wa rehema kwa kutulinda na kutuamsha wote salama na tuko hapa tukiwa na afya njema. Pili ninapenda kuwashukuru ndugu wana habari kwa kuitikia kwa wingi kuhudhuria mkutano huu ambao ni mahususi kwa ajili ya kuwahabarisheni nyinyi kwa umuhimu wenu, ili nanyi mkatusaidie kuihabarisha jamii na umma wa watanzania wote kwa ujumla wake.
Kampuni ya L-VIC Investments Limited ya Dar es salaam pamoja na washirika wetu Kabuhara Beach; Clouds Media Group; Tanzania Airports Authority (TAA); CRDB Bank na TANAPA tumewaiteni kuwahabarisha juu ya jambo kubwa la kiuchumi ambalo kwa dhati ya mioyo yetu tunapenda kumshukuru sana Mh. Dk. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutufungulia uchumi wa utalii katika mikoa yetu hii ya Geita na Kagera lakini kwa Kanda ya Ziwa katika ujumla wake. Hii ni kufuatia kuyapandisha hadhi mapori kadhaa ya akiba na kuyafanya Mbuga za Taifa (National Parks) ambazo sasa zitaruhusu shughuli za uchumi wa utalii kushamiri katika mikoa yetu na Kanda ya Ziwa yote.
Tunapenda kumpongeza Mh. Dk. John Joseph Pombe Magufuli na serikali yake anayoiongoza kwa kudhihirisha kwa vitendo, ndani ya miaka mnne ya uongozi wake ameyafanya mambo makubwa mengi lakini leo tutaongelea sekta ya utalii peke yake:
i. Amelifufua shirika la ndege la Tanzania (ATCL) ambalo mpaka sasa linazo ndege za kati Bombadier (3), madege makubwa Boeing 767 Dreamliner (2) na Airbus 320 (1) na ndege nyingine 3 zimekwishalipiwa zitapokelewa mwanzoni mwa mwaka kesho 2020. Umuhimu wa usafiri wa anga kwa kuwezesha utalii kukua haliwezi kusisitizwa zaidi.
2
ii. Viwanja vya ndege vya zamani vimeendelea kuboreshwa na vipya kujengwa. Viwanja vya
Mwanza, Mtwara vinapanuliwa. Dodoma utajengwa uwanja wa kimataifa. Chato uwanja
umekaribia kukamilika na utakuwa ni chachu kubwa kwa maendeleo ya utalii kwa ukanda
mpya wa utalii wa Kaskazini - Magharibi.
iii. Serikali ya awamu ya tano imeutekeleza bila kupepesa macho Mkakati wa Kukuza Utalii
(Tourism Development Strategy) uliotayarishwa tangu mwaka 1996 na kufanyiwa mapitio
mwaka 2002. Mkakati huo ulisisitiza kuyasisimua mazao ya Utalii katika kanda zote badala
ya Utalii wa Tanzania yenye vivutio vingi na vizuri, kuendeshwa kwenye Ukanda mmoja
wa nchi ambayo inavyo vivutio vya utalii kila sehemu. Kwa mujibu wa taarifa za World
Economic Forum (WEF) ya mwaka 2017 Tanzania ni nchi ya pili duniani yenye vivutio
vingi na vizuri duniani ikiwa nyuma ya Brazil.
iv. Ni serikali ya awamu ya tano ambayo imetekeleza kwa vitendo kuufungua utalii kwenye
kanda za Kusini na Kaskazini – Magharibi kwa kuzitangaza Hifadhi za Taifa za Burigi-
Chato National Park, Rumanyika National Park na Ibanda National Park.
v. Aidha Mh. Dk. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa awamu ya tano mwezi Agosti 2019
aliielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kuitenga (demarcation) upya Seouls Game
Reserve na kuanzisha Mbuga ya Wanyama (National Park) itakayoitwa Mwl. Nyerere
National Park.
Kwa hayo mambo matano yaliyotajwa hapo juu, ni dhahiri Mheshimiwa Rais amedhamiria
kuongeza idadi ya watalii wanaoitembelea nchi yetu na kuongeza mapato yatokanayo na utalii
kwa njia kuu mbili:
i. Kwa watalii kukaa nchini kwa muda mrefu zaidi wakitembelea vivutio ambayo
vimesambaa kila kona ya nchi; au
ii. Kwa kuwavutia watalii wengi zaidi kuitembelea Tanzania ili kuviona vivutio vya utalii
ambavyo vimesambaa kila kona ya nchi.
Hivyo basi ipo kila sababu ya kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa aliyoyatekeleza katika
kipindi cha maiaka yake mmine madarakani. Na njia sahihi ya kumpongeza Mh. Rais ni
kuhakikisha hizo fursa tunazitambua na kuzitumia kwa manufaa ya kujiletea utajiri. Ikumbukwe
kwamba Mh. Rais Magufuli, kwa kauli yake mwenyewe, anayo shahuku kubwa ya
kuwatengeneza mabilionea wa kitanzania na moja ya sekta zenye uwezo mkubwa wa
kuwatengeneza mabilionea ni biashara ya utalii. Licha ya kutengeneza mabilionea sekta ya utalii
inatoa mchango mkubwa katika kutengeneza ajira na kuondoa umasikini wa kipato pasipo
ubaguzi wa jinsia. Utalii unatoa fursa kwa mtu yeyeyote kushiriki.
Kabuhara Beach; Clouds Media Group; Tanzania Airports Authority (TAA); CRDB Bank
na TANAPA tunaungana kumpongeza kwa dhati ya mioyo na kumuunga mkono kwa vitendo
Mheshimiwa Dk. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wetu mpendwa wa Awamu ya Tano ya
Serikali ya Muungano wa Tanzania, kwa uamuzi wake thabiti wa kufungua uchumi wa utalii
kwa kuyabadilisha mapori ya akiba na kuzitangaza mbuga tatu za Wanyama za Burigi-Chato
3
National Park; Ibanda National Park na Rumanyika National Park. Ni dhahiri kwa uamuzi
huo uchumi wa mikoa ya Geita, Kagera na Kanda ya Ziwa kwa ujumla wake utapaa. Basi
shime wananchi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa tumshukuru Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kwa
kuzichangamkia fursa za uchumi wa utalii.
Utalii ni sekta mtambuka ambayo inayo mahusiano na kuhudumiwa na sekta nyingine za uchumi.
Utalii unajulikana kwa kuwa na matokeo chanya na hasi. Kwa uhakika matokeo chanya ni
makubwa kuliko yaliyo hasi. Matokeo hasi ambayo ukiyatambua na kutoa elimu ya ufahamu ni
rahisi kuyahepuka. Na hilo ndilo kusudio la “Lake Victoria Basin Tourism Expo 2019”
likilenga kuongeza ufanisi na manufaa makubwa kwa wananchi ambao ndio watakao endesha
huduma na shughuli mbali mbali za uvunaji wa mazao mbali mbali ya utalii katika ukanda huu
mpya wa utalii uliofunguliwa.
Nini kitafanyika, lini na wapi?
Kama ilivyozoeleka watanzania walio wengi hususani watu wa mkioa ya Kanda ya Ziwa,
wanaoishi na kufanya kazi maeneo mbali mbali humu nchini na kwingineko duniani hurejea
kuungana na familia zao ndugu, jamaa na marafiki kusherehekea sikukuu za Krismass na Mwaka
Mpya. Tumekiona hicho ndicho kipindi sahihi cha kuweza kuwaandalia matukio ya kupeana
ufahamu/uelewa (awareness) kuhusu uchumi wa utalii na fursa zake. Hatua hii inakusudia
kuwawezesha watanzania wa mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Simiyu na Tanzania kwa
ujumla kuuelewa mnyororo wa thamani wa uchumi wa utalii ili waweze kujipanga kuzikamata
fursa za kiuchumi na kutengeneza fedha au kupata ajira. Kwa hiyo ni fursa ya kufanya maandalizi.
Senneca aliyeishi Karne ya 16 anasema “Bahati na pale maandalizi hukutana na fursa”. Nia
ya program hii ni kama msemo maarufu “Ukimpatia mtu samaki utamlisha kwa siku moja.
Lakini ukimfundisha kuvua samaki, atakula milele.”
Ufahamu/ uelewa (Tourism value chain awareness) utajengwa kwa kufanya yafuatayo:
1. Kwa siku 15 kuanzia tarehe 12 Disemba 2019 Gari la matangazo na kusambaza vipeperushi
litazunguka kwenye wilaya zote za mikoa ya Kagera na Geita, kueneza habari za ujio wa
uchumi wa utalii. Pia litahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye
shughuli mbali mbali za “Lake Victoria Basin Tourism Expo 2019”
2. Tarehe 27 Disemba, 2019 washiriki watakaokuwa wamejiorodhesha kwa ajili ya Kongamano
la siku mbili la kujadili Uchumi wa Utalii na mnyororo wake wa thamani, watakwenda
kuzitembelea mbuga mpya za Wanyama kadiri watakavyokuwa wamechagua. Habari kuhusu
National Parks mpya za Burigi-Chato National Park, Rumanyika National Park na Ibanda
National Park, zitawekwa kwenye tovuti ya www.lil.co.tz kuanzia tarehe 25 Novemba 2019
siku ambayo usajili kwa ajili ya kushiriki utafunguliwa kwa muda wa siku 15.
3. Tarehe 28 na 29 Disemba 2019 litafanyika Kongamano la Utalii ambapo mawaslilisho
(Presentations) zitafanyika zikiwashirikisha Wizara ya Maliasili na Utalii kama watunga Sera
4
za Utalii na Miongozo yake, TANAPA ambao ndio wamiliki na wahifadhi wa National Parks
zote. Tourism Confederation of Tanzania na vyama vyake shirikishi wakiwa ni wavunaji wa
utalii kutoka sekta binafsi nao watakuwa na nafasi ya kutoa mhadhara. Aidha washiriki
wengine kutoka tasisi wezeshi za utalii (Tourism facilitation institutions kama TPA, Polisi,
Uhamiaji, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Taasisi za fedha na Kampuni ya Simu
TTCL nazo zitatoa mihadhara kuonyesha zimejipanga vipi kuuwezesha utalii kukua na
kuwanufaisha wananchi na taifa kwa ujumla. Kongamano hilo litafanyika kwenye ukumbi wa
ELCT Bukoba Hotel, Bukoba mjini.
4. Sambamba na Kongamano, washiriki waliorodheshwa hapo juu pamoja na Halmashauri za
Wilaya zote za mikoa ya Kagera na Geita kwa siku tatu kuanzia tarehe 28 hadi 30 Disemba
2019 watakuwa na maonyesho yatakayofanyikia kwenye ufukwe mwanana wa Kabuhara,
Kata ya Kanyangereko, Wilaya ya Bukoba Vijijini.
5. Sambamba na maonyesho hayo litatengwa eno maalumu kwa ajili ya burudani ambapo
wasanii maarufu kama King Kiki (mzee wa Kitambaa Cheupe) na bendi yake Afrika Bara
Moto – Wazee Sugu ya Dar es salaam, Wana Njenje (mabingwa wa mduara) na Msanii
maarufu wa kizazi kipya Nandi watakuwepo Kabuhara kutoa burudani sambamba na wasanii
wengi wa Bukoba.
Mgeni Rasmi:
Tunatarajia kumualika Mh. Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ndiye
awe Mgeni Rasmi. Tumempendekeza huyo kwa sabu kubwa mbili: i. Ni mmoja wetu akiwa ni
mzaliwa wa Kagera anayeishi na kufanya kazi nje ya mkoa wa Kagera (diaspora) ii. Ni mmoja
kati ya watu mashuhuri hapa nchini ambaye hadhi ya program hii inastahili awe Mgeni Rasmi.
Kuhusu uchumi wa utalii:
Uchumi wa utalii ni aina ya biashara ya Uuzaji bidhaa nje ya nchi (export-oriented business)
lakini tofauti yake haihusishi upelekaji wa bidhaa kama “export” za kawaida zilivyo. Watalii
hufika wenyewe katika eneo husika kwa ajili ya kufurahia mazao ya utalii kadiri
yalivyoendelezwa na kutangazwa ili kuwavutia watalii. Ndiyo maana serikali nyingi duniani
uweka juhudi kubwa katika kukuza sekta ya utalii kutokana na umuhimu wake wa kuingiza
mapato ya fedha za kigeni (forex). Fedha zitokanazo na uchumi wa utalii, husaidia katika kuweka
sawa urari wa biashara yaani “Balance of Payments” ambayo ni tofauti kati ya mapato ya mauzo
ya nje na matumizi ya fedha za kigeni kuagiza bidhaa mbali mbali.
Yapo mazao mengi ya utalli ikiwa ni pamoja na utalli wa picha, fukwe, utamaduni, malikale,
historia, mandhari, michezo, mikutano, matamasha n.k Ndiyo maana utalii unaweza kufanyika
popote palipo na uhai wa binadamu kwani kuna vivutio vya asili na vingine vya kutengenezwa
na binadamu.
Utalii ni sekta mtambuka ambayo inayo mahusiano na kuhudumiwa na sekta nyingine za uchumi.
5
Utalii ni sekta yenye kuwa na mguso wa kuleta msongo kwa Utalii unajulikana kwa kuwa na
matokeo chanya na hasi. Kwa uhakika matokeo chanya ni makubwa kuliko yaliyo hasi. Matokeo
hasi ambayo ukiyatambua na kutoa elimu ya ufahamu ni rahisi kuyahepuka. Na hilo ndilo kusudio
la “Lake Victoria Basin Tourism Expo 2019” likilenga kuongeza ufanisi na manufaa makubwa
kwa wananchi ambao ndio watakao endesha huduma na shughuli mbali mbali za uvunaji wa
mazao mbali mbali ya utalii katika ukanda huu mpya wa utalii uliofunguliwa.
Niitumie fursa hii kuwatumia rai wadau wetu mbali mbali ambao tumewatambua na tayari
tumewafikia kwa kuwaandikia barua kuwapa taarifa hizi, shime wahamasike na wajiunge pamoja
nasi ili tushirikiane kumpongeza mpendwa wetu Mh. Dk. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa
awamu ya tano ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maono yake makubwa
kwa nchi yetu, ikiwa ni pamoja na kufanya maendeleo makubwa sekta ya utalii.
Nimalizie kwa kurudia tena kuwashukuru kwa kufika kwa wingi wenu na nirudie kuwakumbusha
kwa kutumia vyombo vyenu vya habari mkaihabarishe jamii kwa usahii na huo ndio uwe
mchango wenu katika kuukaribisha kuusisimua uchumi wa utalii katika ukanda wetu huu.
Asanteni kwa kutusikiliza na sasa kabla ya kukaribisha maswali, nitaomba nitoe yangu ya moyoni
na niwaombe ndugu waandishi wa habari mtusaidie kwenda kutafuta na kupata ukweli kutoka
kwa RAS/ Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Imewasilishwa na:
Anic R. Kashasha
Afisa Mtendaji Mkuu.
L-VIC Investments Limited
Kabuhara Beach, Kanyangereko, Bukoba (V)
Tarehe: 18 Disemba, 2019

Leave A Comment