Lake Victoria Basin Tourism Expo

  • Home
  • /
  • Lake Victoria Basin Tourism Expo [27 Disemba]
Lake Victoria Basin Tourism Expo
Alt
KUWA MDHAMINI WETU
SHIRIKI MAONYESHO
SHIRIKI KONGAMANO

Lake Victoria Basin Tourism Expo itahusisha:

  1. Tour Excursions” Tarehe 27 Desemba 2019 kwa kushirikiana na Kiroyera Tours ya mjini Bukoba washiriki wata pata fursa ya kuzitembelea mbuga mpya tatu za Burigi-Biharamulo National Park; Rumanyika National Park na Ibanda National Park kadiri watakavyo chagua.
  2. Tourism Forum” Kwa siku mbili tarehe 28 & 29 Desemba, 2019 mada kuhusu mnyororo wote wa thamani zitawasilishwa na wataalam mbali mbali kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, TANAPA, TTB, NCCA, TCT na vyama vyake shiriki vyote vikiwemo TATO, HAT, TASOTA, TAHOA, ITTA na ZATI  ,Wakuu wa Mikoa ya Geita na Kagera na Wadhamini wa “Lake Victoria Basin Tourism Expo” Tourism Forum itafanyika kwenye ukumbi wa ELCT Bukoba Hotel, iliyoko Bukoba mjini.
  3. “Expo” Maonyesho ya utalii yatafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 28, 29 na 30 Desemba 2019. Maonesho hayo yatazihusisha Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zote zilizo chini yake, TCT na vyama vyote vilivyo chini yake pamoja na  Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote za Wilaya za Kagera wadhamini wa Lake Victoria Basin Tourism Expo” na pamoja na washiriki wengine watakao jiorodhesha kushiriki. Nafasi ya upendeleo itatolewa kwa wananchi wanaojihusisha na kazi za mikono (Sanaa) kuonyesha na kuuza bidhaa zao bila kulipia gharama za kushiriki. Expo itafanyikia kwenye fukwe ya mchanga mweupe ya Kabuhara, Maruku, Bukoba Vijijini takribani kilomita 20 kutoka Bukoba mjini.
  4. “Event” Burudani itakuwa ni shehemu muhimu ya“Lake Victoria Basin Tourism Expo”Burudani zitatumbuizwa na wasanii mbali mbali wenye mvuto kwa jamii. Mpaka sasa tumekubaliana na msanii King Kiki na Bendi yake  Ya Kapitale Wazee Sugu atashiriki na atatunga wimbo maalumu wa kuhamasisha utalii kwenye Kanda ya Ziwa Victoria. Bado jitihada zinafanyika kumpata msanii mwingine mmoja wa kizazi kipya atakaye toa burudani.

Tarehe za “Lake Victoria Basin Tourism Expo” kuanzia tarehe 27 Desemba hadi 30 Desemba kila mwaka zimechaguliwa mahsusi kwa kuwalenga wananchi wa mikoa ya Kagera na Geita waishio na kufanya kazi nje ya mikoa yao kujenga utamaduni wa kurejea kwa wingi katika kipindi cha sherehe za Krismas na Mwaka Mpya.

Mgeni Rasmi wa kufungua “Lake Victoria Basin Tourism Expo” kwa mwaka 2019 tunamlenga awe Mh. Bashiru Ally Kakurwa, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ambaye ni mwana Kagera ili na yeye apate kushiriki katika kuhamasisha uchumi wa utalii. Mgeni Rasmi wa kufunga tunampendekeza awe Mkuu wa Mkoa wa Geita,  kwa sababu moja kuu, kudhihirisha kwamba “Lake Victoria Basin Tourism Expo” itakuwa ni tukio la kuzunguka katika mikoa ya Kagera na Geita. Hivyo basi mwaka 2020 “Lake Victoria Basin Tourism Expo” itafanyika mkoani Geita.

OUR SPONSORS


EVENT MANAGER

Alt