Alt

Anic Rwegarulila Kashasha
Afisa Mtendaji Mkuu

Tunayo furaha na heshima kukukaribisha kwenye tovuti yetu. Tunaamini utafurahia kutufahamu na kuyafahamu yale tunayoyafanya na malengo yetu ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu. L-VIC Investments Lilimted ni kampuni mpya inayomilikiwa na kuendeshwa na watanzania wenyewe (wazawa). Pamoja na kwamba hii ni kampuni mpya imebahatika kuongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu mwenye uzoefu mkubwa na mapenzi ya dhati ya tasnia ya utalii Bw. Anic Kashasha ambaye picha yake iko hapo juu, akiwa uzoefu wa miaka 32 katika sekta ya utalii.

Mawazo ya kuianzisha L-VIC Investments Limited yalianza baada ya Mh. Dk. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa awamu ya tano ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipozindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato (National Park), kufuatia uamuzi wa serikali mahiri anayoiongoza kupitisha uamuzi wa kuwahamisha wavamizi wa ardhi na majangili kutoka katika mapori tengefu yaliyopo kwenye wilaya za Chato, Bihramulo, Muleba, Ngara, Karagwe na Kyerwa na kuyapandisha hadhi kuwa Hifadhi za Taifa za Burigi – Chato National Park, Rumanyika-Karagwe National Park na Ibanda-Kyerwa National Park.

Kufuatia uamuzi huo wa serikali ya awamu ya 5 chini ya uongozi mahiri wa Mh. Dk. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Anic Kashasha (57) mzaliwa wa Maruku, Bukoba, mkoani Kagera, kwa niaba ya uongozi wa kampuni ya L-VIC Investments Limited, wananchi wote wa mkoa wa Kagera na mikoa yote ya Kanda ya Ziwa anapenda kutoa pongezi na shukurani nyingi sana na za dhati kwa Mheshimiwa Dk. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa awamu ya tano ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa zawadi hiyo kwa mikoa ya Kagera, Geita na Kanda ya Ziwa kwa ujumla wake. Tunahemewa na furaha kwa jinsi uamuzi huo unavyokwenda kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii katika mikoa yote ya Kanda ya Ziwa. Hii ni kwa sababu kubwa zifuatazo:

Aidha, tukiyatambua mazuri ya sekta ya utalii, pia zipo athari za uchumi wa utalii (negative impacts) baadhi yake zikiwa ni:

Yawezekana siyo faida wala madhara yote tumeweza kuyaorodhesha hapa, lakini ni dhahiri kwamba faida zinazoletwa na kuendeleza uchumi wa utalii ni nyingi au kubwa mno kuliko madhara ambayo ukiyajua ni rahisi kuyawekea mikakati ya kuyadhibiti. Moja ya madhara ya utalii ni pale wananchi katika eneo husika ambapo unaendeshwa utalii wao hubaki ni watazamaji (leakages).Basi, kutokana na uzoefu ambao unachanganyika na kipaji kikubwa cha kujenga mawazo alicho nacho Bw. Anic Kashasha akiwa ni mmoja kati ya watu ambao wamewahi kuandika mawazo mbali mbali na kuyawasilisha Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Bodi ya Utalii (TTB), safari hii akajenga mawazo yenye nia ya kuyapungunguza au kuyazuia kabisa madhara ya (leakages) kwa Ukanda Mpya wa Utalii wa Kaskazini – Magharibi. Hili ni jambo ambalo halikuwahi kufanyika kwa Kanda za Utalii (tourist Circuits) zote zilizotangulia.

Katika utekelezaji wa majukumu yetu, mpango wa muda mfupi utakuwa ni kutoa elimu kwa ajili ya kuuelewa mnyororo wa thamani wa sekta ya utalii ili jamii iweze kuzitambua fursa na kuzichangamkia. Katika muda wa kati tutajikita katika kufanya shughuli za kusisimua utalii wa ndani na utalii wa kikanda. Hili linatarajiwa kufanyika kwa kuitumia rasilimali kubwa ya maji Ziwa Viktoria ambalo Bonde lake ni mali ya asili inayomilikiwa na nchi 5 kati ya 6 zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mkakati huu utatekelezwa kwa kuishirikisha kampuni ya Marine Services Company Limited (MSCL). Aidha tunakusudia kuzishirikisha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na taasisi yake ya Lake Victoria Basin Commission, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na TradeMark East Africa. Wizara pamoja na taasisi zote tulizozitaja, tayari tumezipelekea taarifa tukiomba kuanza mazungumzo/ majadiliano.

Katika mipango ya muda wa kati tunakusudia kuanzisha tukio jingine ambalo litakuwa likifanyika katika kipindi cha msimu wa utalii unapofunguliwa kwa nia na lengo la kuongeza idadi ya watalii watakaozitembelea Hifadhi za Taifa za ukanda wa Kaskazini-Magharibi. Hii itakwenda sambamba na mpango wa kudumu wa kutoa elimu ya Utalii. Hapo siku za mbele reli ya kisasa (SGR) inayojengwa itakapokamilika kwa kufika Mwanza, basi tutafanya kazi pia kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania. Hii itakuwa ni katika mipango ya muda mrefu.

Tunapenda kuwashirikisha maono yetu juu ya uchumi wa mkoa wa Kagera ambao unapakana na nchi za Burundi, Rwanda, Uganda, na Kenya kwa kupitia majini, Kenya. Kijiografia mkoa wa Kagera haupo mbali na nchi za D. R Congo na Sudani Kusini kwa umbali, kwani nchi hizo zote zipo karibu na Bukoba kuliko umbali wa kutoka Bukoba kufika Dar es salaam. Kagera ni mkoa wenye hali ya hewa na mandhari nzuri, milima, mabonde na mito na uoto wa asili ulio kijani kwa mwaka mzima, kwa kuwa ni mkoa wenye mvua karibia kwa mwaka mzima.

Njia za usafiri zikifunguliwa hususan baada ya kukamilika kwa meli mbili zinazokarabatiwa kwa hali ya juu, ikiwa meli nyingine mpya na ya kisasa inajengwa ambapo mpango uliopo ni kwamba meli hizo zitakuwa zinazunguka kutoka Mwanza – Bukoba-Port Bell-Kisumu-Musoma na kurejea Mwanza. Usafiri huo wa uhakika na wa gharama nafuu, unatanua sana masoko na kuchochea ongezeko la biashara baina ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, hususani kwa mikoa iliyomo kwenye Bonde la Ziwa Victoria. Kwa hiyo tukiongeza bidii na maarifa ya kufanya kazi, ni dhahiri uchumi wa mkoa wa Kagera na mikoa yote ya Kanda ya Ziwa unakaribia kuanza kupaa. Kagera itainuka tena kiuchumi na kurejea kileleni ambako iliwahi kuwepo hadi kufikia kwenye miaka ya 1970. Ama kweli, kijiografia Kagera imekaa mkao wa Geneva ya Afrika ya ukweli.

Lucius Annaeus Seneca, mwanafalsafa aliyeishi katika Karne ya 16 aliielezea bahati kuwa hutokea pale maandalizi yakutanapo na fursa. (Tafsiri ni ya kwetu). Nukuu “Luck is when preparedness meets an opportunity”. Hivyo kusudio letu ni kuisaidia jamii kuzitambua, kujiandaa na kuzichangamkia ili kunufaika na fursa zinazoambatana na kufunguliwa kwa utalii katika ukanda wa Ziwa Viktoria. Kutokufanya hivyo itakuwa ni kuiandaa jamii kutokushiriki jambo ambalo siyo jema hata kidogo. Kwa hiyo rai yetu ni kwamba jinsi pekee tunavyoweza kumrudishia fadhila Rais wetu mpendwa Dk. John Joseph Pombe Magufuli ni kuhakikisha tunajiandaa na kuzichangamkia fursa hizo. Wachina wanayo misemo mingi lakini hapa tutautumia huu usemao “Kila safari ndefu huanza kwa hatua moja”. Kwa safari hii ya kujiandaa kunufaika na fursa za uchumi wa utalii ambazo zimefunguka, basi ni kuhakikisha tunashiriki kwenye “Lake Victoria Basin Tourism Expo 2019”. Tunakubaliana kwa dhati kabisa na hekima za “Confucius waliosema, nukuu “Give a man a fish and you feed him for a day. But teach a man how to fish and you feed him for a lifetime”. Twende Kazi!

Ni matarajio yetu kuwaona/ kukutana na ninyi kwenye Lake Victoria Basin Tourism Expo 2019.
Wasalaam,


TOURISM DIAGRAMATIC VALUE CHAIN MAPPING DIFFERRENT ROLE PLAYERS

Alt

Dira

Kuwa vinara wa kusisimua utalii ndani ya eneo la Bonde la Ziwa Viktoria kwa maendeleo endelevu ya watu na kukuzabishara,  uchumi na mashirikiano kwa ustawi wa jamii.

Dhima

Kufanya kazi kwa kushirikiana na serikali, taasisi za umma na binafsi na watu wote wenye maono sawa kwa weledi ili kuleta maendeleo endelevu, tukizingatia viwango na ubora.